Posts

NUGGETS OF LOVE

Image
By Abigael Jepng'etich, Form 1 East Love is a universal migraine A bright stain blurring the vision Blotting out sense and reason Such are the symptoms of true love; Leanness, jealousy, laggardness in thought. Sweet omens and nightmares. Listening for a knock, waiting for  a sign .   For a touch of her fingers, in a darkened room, For a searching look, take courage lover, Could you endure such pain at hand?  St. Georges Girls' School, Eldoret  Wisdom in Action. 

SHUKRANI KWAKO MAMA

Image
Na Michelle Jebet, Kidato Cha Tatu  Bahati mi’ nilipata, kwa kutunzwa naye mama, Yeye alinipakata, kwa mikono yake mama, Malezi niliyopata, ni kutoka kwake mama, Katika yangu maisha, shukrani kwake mama,   Nilipendwa naye mama, mwenye moyo mkujufu, Nilibebwa na mama, aliye yeye mchanagamfu, Alinifaidi wangu mama, miye leo ninamsifu, Katika yangu maisha, shukrani kwako mama,   Ye’ alinibembeleza, nikiwa sina amani, Piya ye aliniviza, aliye kama ye nani? Yeye alinituliza, ni yeye ninamwamini, Katika yangu maish, shukrani kwako mama.   Yeye alinifundisha, niwe mi’ mwema daima, Ye alinifurahisha, kwa maneno yake mama, Piya alinijulisha, kuwa niwe na heshima, Katika yangu maisha, shukrani kwake mama.   Mama aliniambiya, nisiwe mimi msumbufu, Kuwa yule safi piya, nisije kuwa mi’ mchafu, Kuwa wa kusadiya, mwenye mkunjufu, Katika yangu maisha, shukrani kwake mama.   Alinipeleka shule, ili nipate elimu, Nisome haya na yale, nipite niwe hakimu, ‘li niwatetee wale, wanaopata dhulumu, Katika yangu

SAUTI YANGU MSIKIE

Image
Na Michele Jebet, Kidato Cha Tatu  Kilio changu hakika, kitafika mwisho lini? Hakika kimeshindika, nitalia hadi lini? Nchi hii yangu hakika, Nisaidieni jamani, Naipasa yangu sauti, isikike kote kote   Kwani uovu humu nchini, pakubwa umeenea, Wapo wengi chinichini, maovu huvumilia, Na wanafahamu dini, badala ya kukemea, Naipasa yangu sauti, isikike kotekote.   Kila pembe humu nchini, ufisadi umezidi, Mambo gani tena haya, tukomeshe ufisadi, Tujikaze pasina haya,na tuache uhasidi, Naipasa yangu sauti, isikike kotekote.   Kila pembe humu nchini, lazidi kila dakika, Hakika tunaumia, mateso kila tabaka, Tukijikaza kuzuia, tusizidi kuteseka, Naipasa yangu sauti, isikike kote kote.   Kuna tena ubaguzi, mbaguano wa kabila, Piya kwa walaazizi, yabidi tuache ghafla, Kwani hili si azizi, kubagua makabila, Naipasa yangu sauti, isikike kotekote.   Amani kila pahala, hakuna kwa urahisi, Kwani wataka mlungula, upate kwa urahisi, Bali nawasihi kila, tuache sasa upesi, Naipasa yangu sauti, isikike kote

HESHIMA

Image
Na Michele Jebet  Kidato cha Tatu  Hakika ni jambo jema, na hili ni yaadhima, Heshima nayo heshima, ina thamani heshima, Heshima  siyo gharama, tusiweke ‘li lawama, Heshima ina maana, tutilie maanani.   Wakubwa kwa wachanga, heshima kitu muhimu, Sasa miye nawaganga, kuwa si kitu kigumu, Na yeyote piya mganga, wenzetu tuwaheshimu, Heshima ina maana, tutilie maanani.   Wanagenzi na’ skulini, staha tuitunze, Walimu nanyi shuleni, heshima na muitunze, Tabibu zahanatini, staha yako uitunze, Heshima ina maana, tutilie maanani.   Staha ni kitu cha bure, tuwe nayo kila mwia, Kitu hiki cha bwerere, kuhifadhi napania, Heshima kitu cha bure, kuwa na’ naazimia, Heshima ina maana, tutilie maanani.   Wadogo tuwapatapo, tujulianeni hali, Wazima tuwa patapo, tuwajulieni hali, Nasi tujiamkapo, tutajua yetu hali, Heshima ina maana, tutilie maanani.   Tukiwa garini hasa, mkubwa wetu kasimama, Ni jukumu letu sasa,kiti si’ kuwaazima, Kwani sisi yatupasa, tuwaonyeshe heshima, Heshima ina maana, tutilie maan

TUSAIDIE MAYATIMA

Image
Na Michele Jebet Kidato cha Tatu  Ninalo swali wapenzi, nipe muda niulize, Menikera wangu wenzi, kwa muda nisieleze, Wana shida wetu wenzi, jamani si’ tuwafaze. Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.   Tuwapatapo yatima, sio kuwa na wazazi, Tuwapatapo yatima, siokuwa na mavazi, Tuwapatapo yatima, wakiwa ni wajakazi, Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.   Watuombapo Amara, tuwe mkono wazi, Waombapo kila mara, chakula hata mavazi, Kwani hakuna hasara, kuwapa piya makazi, Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.   Ataka auni kwako, ni wanadamu kama si’, Tusijali watokako, tuwasaidie sisi, Watoka huku ‘ma huko, sio lengo letu sisi, Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.   Popote tuwapatapo, tusiwe nao hamaki, Chochote watuombapo, sisi tuwapige jeki, Na tuwasaidiapo, Mungu atatubariki, Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.   Ni furaha iliyoje! Mwenzetu kafaidika, Ni bashasha iliyoje! Mwenzetu kafaidika, Nayo nyemi iliyoje, mwenzetu kafaidika, Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.   Kitaka tuish

URAFIKI

Image
                                                       Na Michele Jebet USena ni jambo bora, katika maisha yetu, Usena ni jambo bora, katika shughuli zetu, Urafiki jambo bora, katika gange zetu, Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.   Katika yetu kazini, tuunge si’ urafiki, Nawasihi nyi’ jamani, tusiwe si’ wanafiki, Muda wetu maishani, tukifuata riziki, Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.   Wanagenzi shuleni, tutunze urafiki, Tabibu hospitalini, tutunze urafiki, Nahodha wa baharini, tutunze urafiki, Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.   Katika shida kwetu, rafiki hutupa jibu, Nayo kuelemewa kwetu, wetu msena huwa jibu, Nayo kwenye tabu kwetu, msiri hutupa jibu Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.   Urafiki mazoeya, usuhuba sio geni, Usena husaidiya, urafiki sio deni, Usena huvumiliya, usena haujivuni, Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.   Tukiwa nao wasena, amani tutadumisha, Na kwa yoyote namna, pamoja twajielimisha, Tukiwa nao wasena, hapana na cha kuchosha, Tuhifadhi urafiki, bain

MSENA WANGU

Image
Na Michele Jebet;  Kidato cha tatu Mwenzangu wewe hakika, namwaga jamani mtama, Kilio changu hakika, miye nimeshika tama, Hakika mi nimechoka, maisha ya kusoma, Msena wangu sikia, nikububujie sasa.   Msena wangu kuna nini, mbona we huna amani? Tena ku’ nini, shuleni, kisichokupa amani? Na kama ni masomoni, tuungane si jamani. Niambiye msena basi, kukufaidi miye niko.   Sii kitabu menikera, kusoma nafurahia, Si vyakula menikera, navifurahia pia, Ni mengi yamenikera,  miye nakububujia, Msena wangu sikia, nikububujie sasa.   Mwenzangu nambiye basi, ni nani wakukerao? Je ni mwanafunzi basi, darasani mlio nao, Ama ni walimu basi, lakini wema hao, Niambiye msena basi, kukufaidi miye niko.   Sahibu mi’ nashahidi, shule lako nalo duni, Kuhama mi’ naahidi, kukaa hapa duni Shuleni kwako baridi, kuhama  mi naamini, Msena wangu sikia, nikububujie sasa.   Sahaba ku’ nini tena, niambiye nikariri, Hapana cha kununua, kila kitu ki shwari, Kokoto duniani na, shuleni hili ni shwari, Niambiye msena basi,