TUSAIDIE MAYATIMA

Na Michele Jebet Kidato cha Tatu 

Ninalo swali wapenzi, nipe muda niulize,

Menikera wangu wenzi, kwa muda nisieleze,

Wana shida wetu wenzi, jamani si’ tuwafaze.

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

Tuwapatapo yatima, sio kuwa na wazazi,

Tuwapatapo yatima, siokuwa na mavazi,

Tuwapatapo yatima, wakiwa ni wajakazi,

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

Watuombapo Amara, tuwe mkono wazi,

Waombapo kila mara, chakula hata mavazi,

Kwani hakuna hasara, kuwapa piya makazi,

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

Ataka auni kwako, ni wanadamu kama si’,

Tusijali watokako, tuwasaidie sisi,

Watoka huku ‘ma huko, sio lengo letu sisi,

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

Popote tuwapatapo, tusiwe nao hamaki,

Chochote watuombapo, sisi tuwapige jeki,

Na tuwasaidiapo, Mungu atatubariki,

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

Ni furaha iliyoje! Mwenzetu kafaidika,

Ni bashasha iliyoje! Mwenzetu kafaidika,

Nayo nyemi iliyoje, mwenzetu kafaidika,

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

Kitaka tuishi sote, kwa amani na furaha,

Tuelewane sa’ sote, na taishi kwa furaha,

Tufaane sisi sote, nasi tutapata furaha,

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

Nayo vema iliyoje, ndugu kuishi pamoja,

Nayo raha iliyoje, ndugu kiwa na umoja,

Kwani nyie mwaonaje?, taifa kiwa pamoja,

Tuwafaidi wenzetu, na mola tatufaidi.

 

 Shule la Upili la Mt. Joji

Busara kwa Vitendo! 

Comments

Popular posts from this blog

URAFIKI

SHUKRANI KWAKO MAMA