SHUKRANI KWAKO MAMA

Na Michelle Jebet, Kidato Cha Tatu 

Bahati mi’ nilipata, kwa kutunzwa naye mama,

Yeye alinipakata, kwa mikono yake mama,

Malezi niliyopata, ni kutoka kwake mama,

Katika yangu maisha, shukrani kwake mama,

 

Nilipendwa naye mama, mwenye moyo mkujufu,

Nilibebwa na mama, aliye yeye mchanagamfu,

Alinifaidi wangu mama, miye leo ninamsifu,

Katika yangu maisha, shukrani kwako mama,

 

Ye’ alinibembeleza, nikiwa sina amani,

Piya ye aliniviza, aliye kama ye nani?

Yeye alinituliza, ni yeye ninamwamini,

Katika yangu maish, shukrani kwako mama.

 

Yeye alinifundisha, niwe mi’ mwema daima,

Ye alinifurahisha, kwa maneno yake mama,

Piya alinijulisha, kuwa niwe na heshima,

Katika yangu maisha, shukrani kwake mama.

 

Mama aliniambiya, nisiwe mimi msumbufu,

Kuwa yule safi piya, nisije kuwa mi’ mchafu,

Kuwa wa kusadiya, mwenye mkunjufu,

Katika yangu maisha, shukrani kwake mama.

 

Alinipeleka shule, ili nipate elimu,

Nisome haya na yale, nipite niwe hakimu,

‘li niwatetee wale, wanaopata dhulumu,

Katika yangu maisha, shukrani kwake mama.

 

Mi nikupe kipi mama, kama shukrani kwako,

Sina la kukupa mama, katika fadhila zako,

Na mimi ulisimama, ni shukrani tu kwako,

Katika yangu maisha, shukrani kwako mama.

 

Shukrani kwako mama, Rabuka akubariki,

Yeye akupe neema, kwa kunitendea haki,

Akulinde wewe mama, akufaidi kwa dhiki,

Katika yangu maisha, shukrani kwake mama. 


Mt. Joji, 

Busara kwa Vitendo. 

Comments

Popular posts from this blog

SAUTI YANGU MSIKIE

URAFIKI