SAUTI YANGU MSIKIE

Na Michele Jebet, Kidato Cha Tatu 

Kilio changu hakika, kitafika mwisho lini?

Hakika kimeshindika, nitalia hadi lini?

Nchi hii yangu hakika, Nisaidieni jamani,

Naipasa yangu sauti, isikike kote kote

 

Kwani uovu humu nchini, pakubwa umeenea,

Wapo wengi chinichini, maovu huvumilia,

Na wanafahamu dini, badala ya kukemea,

Naipasa yangu sauti, isikike kotekote.

 

Kila pembe humu nchini, ufisadi umezidi,

Mambo gani tena haya, tukomeshe ufisadi,

Tujikaze pasina haya,na tuache uhasidi,

Naipasa yangu sauti, isikike kotekote.

 

Kila pembe humu nchini, lazidi kila dakika,

Hakika tunaumia, mateso kila tabaka,

Tukijikaza kuzuia, tusizidi kuteseka,

Naipasa yangu sauti, isikike kote kote.

 

Kuna tena ubaguzi, mbaguano wa kabila,

Piya kwa walaazizi, yabidi tuache ghafla,

Kwani hili si azizi, kubagua makabila,

Naipasa yangu sauti, isikike kotekote.

 

Amani kila pahala, hakuna kwa urahisi,

Kwani wataka mlungula, upate kwa urahisi,

Bali nawasihi kila, tuache sasa upesi,

Naipasa yangu sauti, isikike kote kote.

 

Mi’ natamatisha sasa, kwenu nyie viongozi,

Yafaa muongozo ‘sa, kwani nyinyi viongozi,

Komesheni hayo sasa, anzeni kwenye gatuzi,

Naipasa yangu sauti, isikike kote kote.


 Mt. Joji, 

Busara kwa Vitendo 

 

Comments

Popular posts from this blog

SHUKRANI KWAKO MAMA

URAFIKI