MSENA WANGU

Na Michele Jebet; Kidato cha tatu



Mwenzangu wewe hakika, namwaga jamani mtama,

Kilio changu hakika, miye nimeshika tama,

Hakika mi nimechoka, maisha ya kusoma,

Msena wangu sikia, nikububujie sasa.

 

Msena wangu kuna nini, mbona we huna amani?

Tena ku’ nini, shuleni, kisichokupa amani?

Na kama ni masomoni, tuungane si jamani.

Niambiye msena basi, kukufaidi miye niko.

 

Sii kitabu menikera, kusoma nafurahia,

Si vyakula menikera, navifurahia pia,

Ni mengi yamenikera,  miye nakububujia,

Msena wangu sikia, nikububujie sasa.

 

Mwenzangu nambiye basi, ni nani wakukerao?

Je ni mwanafunzi basi, darasani mlio nao,

Ama ni walimu basi, lakini wema hao,

Niambiye msena basi, kukufaidi miye niko.

 

Sahibu mi’ nashahidi, shule lako nalo duni,

Kuhama mi’ naahidi, kukaa hapa duni

Shuleni kwako baridi, kuhama  mi naamini,

Msena wangu sikia, nikububujie sasa.

 

Sahaba ku’ nini tena, niambiye nikariri,

Hapana cha kununua, kila kitu ki shwari,

Kokoto duniani na, shuleni hili ni shwari,

Niambiye msena basi, kukuhifadhi miye niko.

 

Naam muhibu sasa,naafikiana nawe,

Lakini kwa hili sasa, sibadiliki wewe,

Nilichoeleza sasa, kisikutie kiwewe,

Msena wangu sina, nikububujie sasa.

 

Mwandani wangu hakika, tujenge yetu maisha,

Shuleni ukitoroka, utafuta yako maisha,

Twajikaza hakika, tajenga yetu maisha,

Niambiye msena basi, kukuhifadhi miye niko.

 

Mwenzi sa’ sikuhukumu, hakika nimekubali,

Nabaki mi sasa humu, nifaidike kwa ukweli,

Nataka kufuzu humu, ili nije kuwa fali,

Msena wangu sikia, nikububujie sasa.

 

Nashukuru sasa mola, mwenzangu kageuka,

Nitakupa mi fadhila, na tumheshimu labeka,

Tukimheshimu Mola, tutabarikiwa hakika,

Tuungane hili swala, la masomo taridhika. 


Shule  La Upili la Mt. Joji, Eldoret

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SAUTI YANGU MSIKIE

SHUKRANI KWAKO MAMA

URAFIKI