HESHIMA

Na Michele Jebet Kidato cha Tatu 

Hakika ni jambo jema, na hili ni yaadhima,

Heshima nayo heshima, ina thamani heshima,

Heshima  siyo gharama, tusiweke ‘li lawama,

Heshima ina maana, tutilie maanani.

 

Wakubwa kwa wachanga, heshima kitu muhimu,

Sasa miye nawaganga, kuwa si kitu kigumu,

Na yeyote piya mganga, wenzetu tuwaheshimu,

Heshima ina maana, tutilie maanani.

 

Wanagenzi na’ skulini, staha tuitunze,

Walimu nanyi shuleni, heshima na muitunze,

Tabibu zahanatini, staha yako uitunze,

Heshima ina maana, tutilie maanani.

 

Staha ni kitu cha bure, tuwe nayo kila mwia,

Kitu hiki cha bwerere, kuhifadhi napania,

Heshima kitu cha bure, kuwa na’ naazimia,

Heshima ina maana, tutilie maanani.

 

Wadogo tuwapatapo, tujulianeni hali,

Wazima tuwa patapo, tuwajulieni hali,

Nasi tujiamkapo, tutajua yetu hali,

Heshima ina maana, tutilie maanani.

 

Tukiwa garini hasa, mkubwa wetu kasimama,

Ni jukumu letu sasa,kiti si’ kuwaazima,

Kwani sisi yatupasa, tuwaonyeshe heshima,

Heshima ina maana, tutilie maanani.

 

Tamati nimefikiya, nadhani ili mejuwa,

Iwe yetu mazoeya, iwe la kuzingatiwa,

Nadhani tazingatiya, mikono yangu menawa.

Heshima ina maana, tutilie maanani.

 


Mt. Joji

Busari kwa vitendo 

Comments

Popular posts from this blog

URAFIKI

TUSAIDIE MAYATIMA

SHUKRANI KWAKO MAMA