URAFIKI

                                            Na Michele Jebet

USena ni jambo bora, katika maisha yetu,

Usena ni jambo bora, katika shughuli zetu,

Urafiki jambo bora, katika gange zetu,

Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.


 Katika yetu kazini, tuunge si’ urafiki,

Nawasihi nyi’ jamani, tusiwe si’ wanafiki,

Muda wetu maishani, tukifuata riziki,

Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.

 

Wanagenzi shuleni, tutunze urafiki,

Tabibu hospitalini, tutunze urafiki,

Nahodha wa baharini, tutunze urafiki,

Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.

 

Katika shida kwetu, rafiki hutupa jibu,

Nayo kuelemewa kwetu, wetu msena huwa jibu,

Nayo kwenye tabu kwetu, msiri hutupa jibu

Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.

 

Urafiki mazoeya, usuhuba sio geni,

Usena husaidiya, urafiki sio deni,

Usena huvumiliya, usena haujivuni,

Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.

 

Tukiwa nao wasena, amani tutadumisha,

Na kwa yoyote namna, pamoja twajielimisha,

Tukiwa nao wasena, hapana na cha kuchosha,

Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima.

 

Kikomo mimi natia, mengi ya kunena sina,

Hizo sita shikilia, tutunze yetu usena,

Kwa dhati naelezea, tia maanani sana,

Tuhifadhi urafiki, baina yetu daima. 


Shule ya Upili ya Mt. Joji Eldoret

 

 

 

 

  

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SAUTI YANGU MSIKIE

SHUKRANI KWAKO MAMA